Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema yuko tayari kuhukumiwa gerezani kwa kufanya ulaghai kuwaaminisha UMMA wa Watanzania kuwa klabu ya Simba ni kubwa zaidi Tanzania
Aidha kuhusu idadi ya mataji, Manara amesema takwimu alizozitengeneza mwenyewe wakati yuko Simba ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazikuwa sahihi kwani anafahamu Yanga ndio timu yenye mataji mengi zaidi
"Moja ya kazi kubwa niliyoifanya labda ni kuonesha ukubwa feki hiyo dhambi niliitendea vibaya sana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nipo tayari kuhukumiwa hata gerezani kwa kufanya ulaghai wa kufix ukubwa ambao haupo," alisema Manara
Manara amesisitiza yeye ni Mwanayanga kwenye maisha yake hajawahi kuwa Simba na huo ukubwa aliokuwa akiwaaminisha Simba wanao ulikuwa 'feki'