Ni keshokutwa Jumapili pale uwanja wa Benjamin Mkapa, Wananchi wanaanza kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa kuwakaribisha Rivers United katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni
Habari njema kwa Wananchi ni kurejea kwa wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa wakiongozwa na fundi wa mpira Feisal Salum 'Fei Toto'
Ukizungumzia kiungo bora ndani ya ardhi ya Tanzania kwa sasa jina la kwanza katika orodha litakuwa la Fei Toto
Karejea akiwa timamu kabisa kuwapa furaha Wananchi kama alivyofanya wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa
Yanga iko sawa, akina Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Djigui Diarra, Yannick Bangala, Saido Ntibazonkiza na wengineo wamerudi
Yanga imepania kurejea kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kishindo cha aina yake..!


