Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Yanga baada ya kuchelewa kurejea kutoka Zambia.
Chirwa alipewa ruhusa ya kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia mwanzoni wa mwezi Disemba, 2017 lakini amerejea juzi.
Iwapo Kamati ya Nidhamu itampata na hatia huenda akaadhibiwa.
Wakati Yanga ikichukua hatua hizo, Chirwa tayari amesimamishwa na TFF akituhumiwa kwa utovu wa nidhamu.
Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana kutoa maamuzi juu ya tuhuma zinazomkabili pamoja na wachezaji wengine, yeye akidaiwa kufanya matukio ya utovu wa nidhamu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Prisons.

ADVERTISE HERE