Uongozi wa Yanga umepokea taarifa kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kuhusu zuia la mashabiki kuingia uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Rivers United ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga tayari ilikuwa imetangaza viingilio vya mchezo huo lakini kulingana na taarifa ya CAF, Tanzania bado haijafikia viwango vya CAF juu ya protokali ya usimamizi wa ugonjwa wa Uviko-19 hivyo mashabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani
Yanga imeomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza huku ikiwataka mashabiki kushuhudia mchezo huo kupitia Azam Sport 1 HD
ADVERTISE HERE