Baada ya kupoteza mchezo Jumapili, jana Yanga ilirejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili ijayo, Septemba 19 huko Nigeria
Jambo moja la uhakika ni kuwa kama mashabiki wameumia kwa timu yao kupoteza mchezo, basi wachezaji wameumia zaidi
Ari waliyorejea nayo mazoezini jana imetoa taswira kuwa wako tayari kwa mapambano huko ugenini
Zitakuwa dakika 90 za kisasi wakiahidi kurejesha furaha ya mashabiki baada ya mchezo huo
Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya Rivers United kwa bahati mbaya, kwani kama wangetumia nafasi nyingi walizotengeneza, pengine wangeondoka na ushindi usipungua mabao matatu
Sasa wachezaji wanafahamu wanapaswa kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili ili kutinga raundi ya kwanza
Ushindi wa bao 1-0 ugenini pia utapeleka mchezo huo mshindi kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati
Hii ni vita ya kamili inakwenda kupiganwa Nigeria