Hawa Rivers United watajibiwa uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2021
Hawa Rivers United watajibiwa uwanjani

Wengi wetu tumemsikia kocha wa Rivers United akishusha tuhuma kwa Yanga kuwa walipokuja hapa Tanzania walifanyiwa hujuma ikiwa ni pamoja na baadhi ya wachezaji wake kubambikiziwa kuwa wana maambukizi ya uviko-19

Kocha huyo alikwenda mbali kwa kutoa kejeli kuwa wachezaji wa Yanga ni watoto wadogo na huko Nigeria wana uhakika wa kushinda zaidi ya mabao manne

Bila shaka ujumbe huu umewafikia wachezaji na viongozi wa Yanga, huyo kocha wa Rivers majibu anapaswa akutane nayo uwanjani

Kauli zake ni kuichafua Yanga tu, kwani kwa suala la uviko-19 Yanga haihusiki kwa namna yoyote katika vipimo

Kwa kawaida vipimo hivyo vinafanyika chini ya uangalizi wa CAF wenyewe na usimamizi wa Serikali ya nchi ambayo mchezo unapigwa

Yanga tayari wanazo taarifa ya hujuma ambazo wamekuwa wakizifanyia timu pinzani katika michuano ya CAF huko Nigeria

Maneno yake ni kama kujaribu kuhalalisha mambo maovu ambayo wamepanga kuifanyia Yanga kwa kivuli cha kulipa kisasi

Hata hivyo hawataweza kwani Yanga ilifahamu mapema kuhusu uovu huo na ndio maana mpaka sasa hawafahamu Yanga itasafiri lini kwenda Nigeria, na hawatafahamu

Wao wasubiri kuiona Yanga ikiingia uwanjani na baada ya mchezo Wananchi wataondoka usiku huo huo kurejea Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’