Tuko tayari kuiwakilisha nchi Nigeria - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2021
Tuko tayari kuiwakilisha nchi Nigeria - Manara

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema pamoja na ugumu wa mchezo dhidi ya Rivers United utakaopigwa Nigeria Jumapili, wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi

Akizungumza na Wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Manara amesema wanatambua mechi za ugenini zina mambo mengi ya nje ya uwanja lakini wamejipanga kukabiliana nayo

"Tunaenda kucheza mechi ambayo kwa vyovyote vile itakuwa ngumu, mechi za ugenini kwenye ligi ya mabingwa siku zote huwaga ni ngumu na hilo jambo tunalitarajia"

"Tunajua mechi za ugenini zina visa na mikasa mingi, kisaikolojia tumejipanga na tumejiandaa na hilo na ndiyo maana tulituma watu imara wakufanya maandalizi yote kabla ya timu kufika," alisema Manara

Manara amesema Yanga itaondoka nchini leo majira ya saa mbili usiku na itafika Nigeria saa tano usiku (saa saba) kwa saa za Tanzania

Katika hatua nyingine, Mtendaji wa Yanga Senzo Mazingisa ambaye yuko nchini Nigeria, amesema maandalizi kwa ajili ya mapokezi ya timu yako tayari

Pamoja na changamoto ya hujuma za hapa na pale, Senzo amesema wako tayari kukabiliana na mazingira ya aina yoyote

"Nimefika toka Jumatatu na kila kitu kimeenda sawa kuhusu hujma hua zipo tu haziwezi kukosa ila tunajitahidi kufanya kila tunaloweza ili tukabiliane nazo, lakini vizuri tunasubiri timu ifike kwanza halafu mengine yatafuata"

"Kila kitu kipo sawa kama ilivyokuwa inafanyika huko nyuma katika mashindano ya kimataifa na kwa upande wetu tupo sawa, tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa balozi kilichobaki tunasubiri Mechi tu," alisema Senzo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’