Yanga, Singida United kukamilisha ratiba, Simba, URA hapatoshi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2018
Yanga, Singida United kukamilisha ratiba, Simba, URA hapatoshi
Hatua ya makundi za Kombe la Mapinduzi 2018 inahitimishwa leo kwa mechi mbili, vigogo Simba na Yanga wakimenyana na URA na Singida United.

Simba SC wataanza kupambana na timu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) Saa 10:30 jioni kabla ya Yanga SC kumenyana na Singida United kuanzia Saa 2:15 usiku, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Yanga na Singida wamekwishafuzu Nusu Fainali na leo watakuwa wanapambana kuwania uongozi wa Kundi B baada ya wote kushinda mechi zao zote nne za awali.

Mchezo wa Simba na URA ndio unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote kuwa na nafasi wa kufuzu hatua ya nusu fainali.

Wakati URA ikihitaji sare tu, Simba ni lazima ishinde ili itinge nusu fainali.

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masudi DJuma amesema timu yake itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi.

Kwani matokeo tofauti na ushindi yataipa Simba tiketi ya mapema ya kurejea nyumbani kutoka kwenye michuano hiyo ambayo mwaka uliopita ilitinga fainali.

Michezo yote itaonyeshwa na kituo cha televisheni cha Azam Sport 2.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’