Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka dimbani huko Nigeria kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga raundi ya kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri kwa saa za Nigeria ambapo kwa Tanzania itakuwa ni saa 12 jioni
Jana jioni Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Adokiye, mahali ambapo mchezo huo utapigwa leo
Msemaji wa mabingwa hao wa kihistoria Haji Manara amesema wamekamilisha maandalizi yao na wako tayari kwa mchezo huo
Amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga pamoja na Watanzania wazalendo kuwaombea ili waweze kupata ushindi
Aidha kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' amesema walisahihisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam wakiahidi kutumia nafasi watakazotengeneza katika mchezo wa leo
Rivers United wamekataa mchezo huo kuonyeshwa katika runinga pamoja na kutangazwa katika redio huku wakigoma hata kuruhusu matangazo kupitia mitandao ya kijamii
Uongozi wa Yanga umeahidi kuwa watatoa taarifa za mchezo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii
Kila la kheri Yanga, Kila la kheri timu ya Wananchi..