Ni mshambuliaji anayeipenda klabu ya Yanga, mashabiki pia wanampenda sana
Heriter Makambo alipata majeraha ya kuchanika juu ya jicho lake katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rivers United uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Lakini leo atawaongoza makamanda kwenye mchezo wa marudiano huko Nigeria
Yanga inahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili, Makambo amesema wamejipanga kushinda leo
"Tumejiandaa vizuri, tunafahamu hatukupata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza lakini huu ni mpira wa miguu na lolote linaweza kutokea. Kama wao walifunga goli moja sisi tutawafunga magoli mawili hapa," alisema Makambo
Mchezo utapigwa kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Tanzania
ADVERTISE HERE