Kiungo Mukoko Tonombe amesema licha ya kutofanya vizuri katika michezo miwili ya ligi ya mabingwa, wana imani kubwa watakuwa na msimu mzuri
Aidha, Mukoko amesema wamejipanga kupata ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Msimu huu tuna timu nzuri licha ya kuwa hatujawa na mwanzo mzuri katika michezo yetu miwili ya kwanza mbele ya mashabiki wetu"
"Tuna imani kubwa na timu yetu na mipango ambayo tunayo kwa msimu ujao. Tutacheza dhidi ya Simba Septemba 25, ni mchezo mgumu lakini kama kikosi tumejipanga vizuri na naamini kuwa tutaibuka na ushindi ," alisema Mukoko
Baada ya kurejea kutoka Nigeria jana, kikosi cha Yanga kilielekea moja kwa moja kambini, Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Simba