Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo ametangaza viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa 11 jioni kuwa VIB ni Tsh 30,000/-, VIP C ni Tsh 20,000/- na Mzunguuko ni Tsh 10,000/-
Aidha Ndimbo amesema hakutakuwa na tiketi za VIP A kwa kuwa nafasi hizo zitatolewa kwa mwaliko hivyo kwa wale ambao watapenda kukaa majukwaa ya VIP A wanapaswa kuwasiliana na TFF
Akizungumza maandalizi ya kuelekea mchezo huo, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wako tayari kwani mchezo huo ulifahamika mapema
"Baada ya kurudi kutoka Nigeria na timu imeingia kambini moja kwa moja, mchezo huu tulikuwa tunaujua kabla ya msimu kuanza kwahiyo tumejipanga vizuri"
"Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hata wale waliokuwa majeruhi wamepona na wapo tayari"
"Kuhusu motisha ipo na wakati tunatoka Nigeria wachezaji walikuwa wanazungumza kuhusu mechi ya dabi na morali ipo juu, hakuna namna ya kuacha kuchukua Ngao ya Jamii," alisema Bumbuli