Yanga haikuanza vizuri msimu kwa kuondoshwa mapema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Wananchi wamerejea wakiwa na ari, Jumamosi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani zao Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii
Huu ni mchezo ambao umeingia katika akili za wachezaji, wanachohitaji ni ushindi tu
Pamoja na kuondoshwa mapema katika ligi ya mabingwa, Yanga imenufaika na mechi mbili walizocheza dhidi ya Rivers United
Zilikuwa mechi zenye ushindani ambazo hakuna shaka zimewaongezea wachezaji kujiamini kuelekea mchezo huo
Kocha Nasreddine Nabi amesema vijana wake wako sawasawa na wana matumaini makubwa ya kushinda Jumamosi
ADVERTISE HERE