Kuna watu hawaamini baada ya Bodi ya Ligi kutoa takwimu za mahudhurio ya mashabiki na mapato ya klabu katika msimu uliopita
Yanga imeongoza katika takwimu zote, licha ya kuwa mabingwa hao wa kihistoria wana takribani misimu minne hawajashinda taji la ligi kuu
Katika hali ya kawaida, wengi walitarajia Simba ambayo imekuwa na mafanikio kwa misimu minne mfululizo huku ikijinadi kuwa sasa ndio klabu kubwa zaidi Tanzania, ukubwa wao ulipaswa kuonekana katika takwimu hizo
Ni Yanga iliyodhihirisha ukubwa wake licha ya kuwa imetoka katika kipindi kigumu sana
Huo ni mwanzo tu, matarajio ni kuona takwimu za kutisha zaidi katika msimu huu kutokana ubora wa kikosi ambacho Yanga wanacho
Yanga ni timu ya kihistoria, haikuitwa timu ya Wananchi kwa bahati mbaya