Ramadhan Kayoko ndiye mwamuzi wa kati katika Mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Watani Wawili, Simba SC dhidi ya Yanga SC siku ya Jumamosi, Septemba 25 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kayoko atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba moja, Frank Komba, namba mbili ni Soud Lila na mwamuzi Akiba na Herry Sasii.
Kayoko alikuwa mwamuzi wa kati Simba SC ilipocheza na TP Mazembe kwenye Simba Day 2021 vile vile alisimamia pambano kati ya Yanga dhidi ya Zanaco Fc kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi
ADVERTISE HERE