Majira ya saa 11 jioni, kikosi cha Yanga kitashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani zao Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii
Ni mchezo unaoashiria ufunguzi wa msimu wa ligi kuu na michuano ya kombe la FA (2021/22)
Kwa Yanga huu ni mchezo muhimu kupata ushindi hasa baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya awali
Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili, wachezaji wote wako katika afya nzuri ikiwemo wale waliokuwa majeruhi
Hata hivyo Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, wakati akizungumza na Wanahabari jana alisema kuwa mlinzi Yassin Mustafa na kiungo Mapinduzi Balama hawatakuwa sehemu ya kikosi leo kwa kuwa bado hawako 'fit'
Katika mchezo huo, mashabiki wa Yanga watarajie kuwaona Shabani Djuma, Khalid Aucho na Fiston Mayele ambao walikosa michezo ya ligi ya mabingwa baada ya ITC zao kuchelewa
Aidha kiungo Mukoko Tonombe nae hatakuwa sehemu ya mchezo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba msimu uliopita
Yanga imedhamiria kushinda mataji yote ya ndani msimu huu, leo ni mtihani wao wa kwanza kudhihirisha utayari wao katika kutimiza dhamira hiyo
Kila la kheri Wananchi...!