Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba hapo jana na kufanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii, kikosi cha Yanga leo kinarudi mazoezini Avic Town kukamilisha maandalizi ya mwisho tayari kwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Jumatano, Septemba 29 katika uwanja wa Kaitaba
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema ni furaha kushangilia taji la kwanza msimu huu lakini hawana muda wa kupoteza, leo wanarejea mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar
"Mwanzo mzuri, Kikombe cha kwanza kimepatikana, lakini kesho (leo) tunarudi mazoezini kujiandaa na mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Kagera Sugar tujiandae vizuri ili tuimarike zaidi", alisema Kaze


ADVERTISE HERE