Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka katika dimba la Kaitaba, Bukoba kuwakabili wenyeji wao Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga msimu huu, mabingwa hao wa kihistoria wakipania kusaka ubingwa wa 28
Yanga iko Kagera tangu Jumatatu ikijiwinda na mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo huo, wakiwa na matumaini ya kuondoka na alama zote tatu
Baada ya kushinda Ngao ya Jamii kwa kuwachapa watani zao Simba mwishoni mwa wiki iliyopita, Wananchi wamepania kuendeleza moto huo wa ushindi kwenye ligi
Kila la kheri Wananchi..!
ADVERTISE HERE