Katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Yannick Bangala alitumika kama kiungo mkabaji
Leo Bangala amerejeshwa katika nafasi ya ulinzi akiwa mbadala wa Bakari Nondo Mwamnyeto aliyeumia kidole wakati wa maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Bangala anaweza kupigiwa kura yanyota wa mchezo leo kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika safu ya ulinzi
Alishirikiana vyema na Dickson Job utadhani wawili hao wamecheza pamoja kwa misimu kadhaa
Wote wako vizuri miguuni, wakiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kuanzisha mashambulizi
Bangala ameongeza ubora katika eneo la ulinzi huku Mganda Khalid Aucho akiongeza utulivu katika eneo la kiungo

Kwa hakika wachezaji hawa wameibadili kabisa Yanga hasa katika umiliki wa mpira
Yanga ilikuwa na kipindi cha kwanza bora sana leo, ni ushindi mzuri ambao utaisaidia timu kuelekea mchezo dhidi ya Geita Gold Jumamosi