Damu changa Yanga zilivyon'gara kombe la Mapinduzi

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
9 Jan 2018
Damu changa Yanga zilivyon'gara kombe la Mapinduzi
Michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofika kwenye hatua ya nusu fainali visiwani Zanzibar imefichua hazina kubwa ya wachezaji vijana walio kwenye kikosi cha Yanga.

Wakati michuano hiyo ilipoanza hofu kubwa ilionekana kwenye nyuso za wadau walioamini kukosekana kwa wachezaji muhimu huenda kungeifanya Yanga iage michuano hiyo mapema. Lakini haikuwa hivyo.

Yanga imetinga nusu fainali 'kibabe' kwa kushinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja dhidi ya Singida United iliyokwenda Zanzibar na kikosi cha maangamizi!

Badala yake timu kama Simba iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo imejikuta ikiiacha Yanga, Azam FC na Singida United Zanzibar na yenyewe ikiwa ya kwanza kurejea Bara.

Lakini michuano hiyo imekuwa na faida kubwa kwa Yanga pengine kuliko timu nyingine zote zilizoshiriki.

Mtindo uliotumiwa na benchi la ufundi chini Shedrack Nsajigwa na Noel Mwandila wa kutokuwa na kikosi cha kwanza kwa ajili ya michuano hiyo, umefichua uwezo wa wachezaji vijana ambao hawakuwa wakipata nafasi awali.

Hapa tuwaangalie wachezaji wachache ambao bila shaka michuano hii inaweza kuwapa nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga.

Ramadhani Kabwili
Kuna mwenye shaka na huyu bwana mdogo? Uchezaji wa Kabwili unanikumbusha mwishoni mwa miaka ya 90 wakati huo Juma Kaseja alipokuwa anaibuka

Kabwili amedhihirisha umri wake sio kitu. Anaweza kucheza katika mechi yoyote ya ushindani.

Huyu ndiye atakuja kuwa Tanzania One wa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Kaseja kama kiwango chake kitaendelea kulindwa.

Makka Edward
Michuano hii imeweza kudhihirisha ubora wa kiungo huyu chipukizi aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili cha Yanga (Yanga B).

Makka ameonyesha kiwango cha hali ya juu. Ameweza kumudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji na bila shaka kijana huyu yuko tayari kuitumikia Yanga kiushindani.

Said Juma Makapu
Makapu yuko katika kikosi cha Yanga msimu wa tatu sasa. Mara nyingi amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji.

Hata hivyo msimu huu hakuweza kupata nafasi baada ya kusajiliwa Papi Tshishimbi huku Pato Ngonyani akiwa chaguo la pili.

Lakini Makapu amedhihirisha anaweza kucheza vizuri zaidi akiwa mlinzi wa kati pengine kuliko hata akiwa kiungo mkabaji.

Ilikuwa ajabu wakati ule Yanga inalalamika kuwa na uhaba wa walinzi wa kati huku benchi kukiwa na Said Juma.

Michezo miwili aliyocheza 'sentahafu' dhidi ya JKU na Zimamoto imedhihirisha Makapu anamudu kucheza nafasi hiyo bila wasiwasi wowote.

Ana 'ball control' nzuri, kimo chake ni kizuri kwa beki, ana maamuzi sahihi, ni mzuri katika kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma kwani pasi zake ndefu nyingi zinafika.

Said Mussa
Mussa ameonekana kuzoea kwa haraka mikiki mikiki ya wakubwa licha ya umri wake kuwa mdogo.

Tayari wengi wameanza kumtabiria kuwa mbadala halisi wa Simon Msuva.

Machachari yake yalimfanya afanyiwe sana madhambi na walinzi wa timu pinzani kwenye michuano hii kupelekea akaumia mkono.

Ni habari njema kusikia tayari amepona majeraha yake na yuko tayari kuitumikia Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya URA kesho.

Yohana Nkomola
Wakati Yanga ilipomsajili kipindi cha dirisha dogo la usajili wapo walioponda usajili huo na kudai Yanga inasajili watoto badala ya kusajili washambuliaji wa maana.

Licha ya umri wake kuwa mdogo, amedhihirisha kuwa yeye ni mshambuliaji wa maana. usumbufu wake pale mbele umekuwa ukiwapa wakati mgumu walinzi wa timu pinzani.

Katika michuano hii amepachika bao moja na ameonyesha ushirikiano mzuri anapocheza na fundi Ibrahim Ajib.

Juma Mahadhi
Kabla ya kuanza michuano hii, Mahadhi 'alitubu' na kuomba apewe nafasi huku akiahidi kutowaangusha tena WanaYanga waliokuwa na imani kubwa kwake aliposajiliwa kutoka Coastal Union misimu miwili iliyopita.

Mahadhi ameonyesha utofauti kwenye michuano hii. Amefunga mabao mawili na kutengeneza bao moja huku akisababisha mpira wa adhabu uliozaa bao la Yanga dhidi ya Singida United jana.

Mahadhi ameonyesha kujituma, anarudi kusaidia ulinzi pale inapolazimu, ameachana na ule mpira wa 'anao anao' anatoa pasi kwa wakati sahihi na anapiga krosi wakati sahihi.

Huu ni mwanzo mzuri kwake na kwa klabu ya Yanga mwaka huu.

Yanga sasa ina idadi kubwa ya wachezaji wanaoweza kucheza nafasi zaidi ya moja hivyo kuondoa hofu linapotokea swala la wachezaji kuumia.

Pato Ngonyani, Makapu na Tshishimbi hawa ni viraka.

Ngonyani na Makapu wanaweza kutumika kama walinzi wa kati au viungo wakabaji wakati Tshishimbi anamudu namba zote za kiungo.

Benchi la Ufundi la Yanga chini ya Kocha George Lwandamina wanahitaji pongezi kwa kazi nzuri ya kujenga kikosi imara cha vijana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’