Huu mchezo hautaki hasira, watulie

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2021
Huu mchezo hautaki hasira, watulie

Msimu wa 2018/19 aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya soka la Vijana, aliwahi kusema kuwa kuna timu zilikuwa zikiahidiwa fedha pale zilipoifunga au hata kutoka sare na Yanga

Zahera alibainisha kuwa taarifa hizo walikuwa wakipewa na watu wa ndani wa timu husika wenye mapenzi na Yanga

Hakuna kiongozi wa Yanga aliyelalamikia jambo hilo hata pale Mkuu wa mkoa wa zamani wa Dar es salaam Paulo Makonda alipowazawadia KMC Tsh Milioni 20 baada ya kuifunga Yanga

Kimsingi sio kosa mtu kuahidi kutoa fedha kwa timu anayoipenda kama itapata ushindi au hata kutoka sare

Hii inaitwa hamasa, kwa Yanga na Simba hili ni jambo la kawaida. Mo amekuwa akitoa fedha kwa wachezaji wa Simba kila wanapofanya vizuri katika mechi zao na ni hivyohivyo kwa GSM pale Yanga inapofanya vizuri

Sasa inakuwaje kuna watu wanalalamika pale Mkuu wa mkoa wa Mara alipotoa ahadi kuwapa fedha Biashara United kama wangeshinda au kutoka sare dhidi ya Simba?

Kuna kosa gani kama mlezi wa Dodoma Jiji atatoa ahadi kwa timu yake kama itashinda au hata kutoka sare?

Ahadi hizi zina tofauti gani na zile zinazotolewa na mabosi wa Yanga na Simba kwa timu zao zinaposhinda?

Hao wanaolalamika hawazitendei haki hizi timu nyingine, wao wanafanya lakini wakifanya wenzao wanaona ni tatizo

Kimsingi hili ni jambo zuri kwa sababu lina manufaa ya moja kwa moja kwa wachezaji pale wanapotimiza ahadi

Timu zijipange, zicheze mpira uwanjani, kulalamika ni dalili ya kushindwa

Miaka ya nyuma Yanga ilikuwa kinara wa kulalamika kutotendewa haki katika mambo mengi lakini msimu huu Wananchi wamesema kulalamika sasa basi

Mpira uchezwe uwanjani huku Mamlaka za usimamizi wa soka zikihakikisha zinatimiza wajibu wao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’