Katika mchezo dhidi ya Geita Gold uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana, Yanga ilitengeneza nafasi 11 za kufunga mabao, nafasi iliyotumika ni moja tu
Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mrefu, kama washambuliaji wangekuwa makini angalau kwa asilimia 50 tu, basi wangeweza kufunga hata mabao matano
Achana na yale mabao mawili yaliyofungwa lakini mwamuzi msaidizi akayakataa kwamba ni offside, Yanga ilikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi
Jambo moja la uhakika ni kuwa sasa Yanga inatengeneza nafasi nyingi, changamoto iliyobaki ni matumizi ya nafasi hizo
Kocha Nasreddine Nabi amesema wanakwenda kuweka kambi Arusha wakati wa mapumziko ya Michuano ya Kimataifa, ameahidi kufanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza
Watakaporejea kuikabili KMC Oktoba 19, watakuwa bora zaidi
Kwa jinsi Yanga inavyocheza, inaogopesha! siku watakayokuwa na usahihi wa matumizi ya nafasi, kuna timu zitaondoka na kapu la magoli