Kiungo wa Yanga Zawadi Mauya amekiri ushindani wa kupata nafasi msimu huu umekuwa mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji wageni waliosajiliwa
Akiwa anacheza eneo la kiungo, Mauya anakabiliwa na changamoto ya kupata nafasi mbele ya Yannick Bangala, Mukoko Tonombe na Khalid Aucho
Mauya ambaye msimu uliopita alikuwa tegemeo katika eneo hilo, msimu huu ameuanza kwa kusuasua kwani hakufanya vizuri sana katika michezo aliyopewa nafasi
Hata hivyo amesema uwepo wa wachezaji bora, unampa ari ya kujituma ili kuwa bora zaidi na kujihakikishia nafasi ya kucheza
"Wachezaji wa kigeni kuna kitu wameongeza, ukweli wanatupa changamoto kubwa. Kuna mambo tunajifunza kupitia changamoto hizo. Ukitaka kuwa bora lazima upitie changamoto mbalimbali. Kwa klabu ni jambo jema kuwa na wachezaji bora katika kutimiza malengo," alisema Mauya
Mauya alitua Yanga akitokea klabu ya Kagera Sugar msimu wa 2019/20 ambapo katika msimu huo aliibuka kuwa kiungo bora wa ligi