Nsajigwa ajipanga kuidhibiti URA leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Jan 2018
Nsajigwa ajipanga kuidhibiti URA leo
Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa kwenye mchezo wa leo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi watakuwa makini baada ya kugundua mbinu za wapinzani wao URA.

Nsajigwa, alisema kuwa watahakikisha wanakuwa makini kwenye safu yao ya ulinzi na viungo hasa kutokana na URA kutumia mfumo wa kujihami na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

“Tumewaona kwenye mchezo wao dhidi ya Simba, ni timu nzuri yenye wachezaji wepesi, tutakabiliana nao kwa umakini mkubwa, ili tuweze kusonga mbele,” alisema Nsajigwa.

Alisema kuwa wanafahamu URA watakuja na mtindo wa kujihami huku wakitegemea mashambulizi ya kushtukiza kuwaadhibu, lakini watakuwa makini na hilo.

Wakati Yanga ikiingia kwenye hatua hiyo baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi B nyuma ya Singida United, URA wenyewe wametinga hatua hiyo baada ya kuongoza kundi A mbele ya Azam FC ambao nao wataumana na Singida United kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa usiku.

Timu hiyo kutoka Uganda, imeonekana kuwa na nidhamu kubwa kwenye kujilinda huku wakiwa wazuri kwenye mashambulizi ya kushtukiza.

Kwenye mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Simba ambao walikuwa wakihitaji sare kutinga nusu fainali, URA ilifanikiwa kuwabana Simba na kupata ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo wa leo utakaoanza majira ya saa 10:00 jioni, Yanga wanapaswa kuwa makini katika safu yao ya ulinzi kuhimili mshambulizi ya kushtukiza ya Waganda hao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →