Mashabiki wa Yanga walizoea kumuona Farid Mussa akicheza kama mshambuliaji wa pembeni lakini sasa anapewa majukumu tofauti
Katika michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold, Farid alitumika kama kiungo mchezeshaji sambamba na Khalid Aucho
Ameendelea na majukumu hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU hapo jana, Yanga ikishinda bao 1-0
Farid ameonyesha uwezo mkubwa katika kusambaza mipira na kuifanya timu iwe na umiliki mkubwa wa mpira
Nabi amemuamini sana Farid tangu mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba akitoa pasi ya bao lililofungwa na Fiston Mayele
Huu unaweza kuwa msimu mzuri kwake kama ataendeleza kile anachokifanya sasa
ADVERTISE HERE