Ukizungumzia kiungo bora kwa sasa ndani ya ardhi ya Tanzania, lazima utaje jina la Feisal Salum 'Fei Toto', fundi wa mpira kutoka visiwani Zanzibar
Fei Toto wa sasa ni tofauti kabisa na yule uliyemshuhudia katika msimu uliopita kabla ya ujio wa kocha Nasreddine Nabi na nyakati zote tangu aliposajiliwa na Yanga
Fei Toto wa sasa amekomaa, shukrani za kipekee anastahili kocha Nabi aliyembadili kuwa mchezaji tofauti sana
Yeye ndio injini ya Yanga pamoja na timu ya Taifa, anabeba mpango wote wa mchezo anapokuwa uwanjani
Ni mchezaji ambaye kwa kweli hastahili kuendelea kucheza soka barani Afrika. Kocha wa zamani wa timu ya Taifa Emmenuel Amunike aliwahi kusema wazi kuwa Fei Toto anaweza kucheza FC Barcelona klabu ambayo yeye (Amunike) akiwahi kuitumikia
Ni suala la muda tu, fundi huyu wa mpira ataweza kudhihirisha maoni ya Amunike na makocha wengine ambao wamemtabiria kufanya mambo makubwa
Kuhimu kwake ni kuendelea kujituma na kufuata maelekezo anayopewa na Walimu wake
Huu ndio wakati wake wa kutimiza ndoto ya kwenda kusakata kabumbu barani Ulaya