Yanga imeangushiwa 'jumba bovu' faini ya CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2021
Yanga imeangushiwa 'jumba bovu' faini ya CAF

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya dola 5,000 klabu ya Yanga kwa kilichoelezwa kuvunja baadhi ya sheria na taratibu za mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika walioucheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria

Adhabu hiyo imetolewa na kamati ya Nidhamu ya CAF kutokana na malalamiko ya klabu ya Rivers United juu ya baadhi ya viongozi wao kughasiwa na walinzi wa uwanjani (Stewards) na baadhi ya mashabiki kuingia uwanjani wakati mchezo huo ambao ulipaswa kuchezwa bila mashabiki

Lakini ukifuatilia kwa undani utabaini katika makosa yaliyoainishwa na CAF, Yanga haihusiki na masuala yake moja kwa moja

Yanga haihusiki na ulinzi wa uwanja, haifanyi vipimo vya Covid 19, haina mamlaka ya kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani na hata siku ya mchezo ilitoa taarifa ya kuwaomba radhi mashabiki wake baada ya CAF kuwazuia kuingia uwanjani

Wenye dhamana ya masuala yote ni TFF kwa kushirikiana na wamiliki wa uwanja wa Benjamin Mkapa

Na hata ukiangalia taarifa ya CAF mpaka mwisho utaona TFF wameonywa kwa kujitokeza kwa matukio mbalimbali yasiyohusiana na mchezo wa Yanga na Rivers ambayo yamelalamikiwa na klabu mbalimbali zilizokuja kucheza Tanzania

Malalamiko ya harufu vyumbani yalianza msimu wa 2018/19 wakati Simba ikishiriki michuano ya ligi ya mabingwa. Zipo timu ziligoma kuingia vyumbani kutokana na harufu kali

Yanga ni miongoni mwa timu zilizolalamikia harufu vyumbani na hata Dodoma Jiji msimu uliopita waligoma kuingia vyumba vya kubadilishia nguo wakati wakicheza na Simba kutokana na harufu kali

Msimu uliopita mambo haya yaliendelea, matukio ya wachezaji wa timu pinzani kuzuiwa kupitia vipimo vya covid yakashamiri

Kwa ufupi Yanga imeadhibiwa kwa makosa ambayo pengine yalifanyika huko nyuma na mengine yalifanyika pasipo wao kuwa na mamlaka ya usimamizi wa moja kwa moja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’