Uongozi wa Yanga umethibitisha kupokea barua pepe kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) juu ya faini waliyopigwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na klabu ya Rivers United dhidi yao
Kupitia kwa mkurugenzi wa uwekezaji GSM Injinia Hersi Said, amesema kuwa hadi ijumaa ya wiki hii watakuwa wamelipa faini hiyo kiasi cha TShs million 11
Hata hivyo Injinia Hersi amesema wataiandikia barua CAF kupitia TFF kuomba ufafanuzi wa faini iyo
"Tumezipokea taarifa kutoka CAF za kupigwa faini kwa sababu kuwaruhusu baadhi ya mashabiki kuingia uwanjani. Tutailipa faini hiyo hata hivyo nasi tayari tulishafungua malalamiko yetu dhidi yao Rivers united tulivyokwenda kwao Nigeria walitufanyia hujma za wazi wazi kwa wachezaji wetu pamoja na viongozi
"Ni matumaini yetu CAF watachukua hatua kama walivyofanya kwa malalamiko yaliyotolewa na Rivers United dhidi yetu," alisema Hersi
Miongoni mwa matukio ambayo Yanga walifanyiwa Nigeria ni pamoja na msafara wao uliokuwa na viongozi kuzuiwa kuingia uwanjani
Pia jaribio la kuwazuia baadhi ya wachezaji wasicheze kwa kisingizio cha uviko-19 licha ya kuwa wachezaji wote walipimwa na hawakuonekana na maambukizi hayo
Pia hawakuweza kutumia vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kuchelewa kupewa funguo za vyumba hivyo lakini pia wakabaini havikuwa na taa