Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewatahadharisha nyota wake kuwa wanapaswa kuweka mbele maslahi ya timu na sio yao binafsi
Baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU, Nabi hakufurahishwa na tabia ya 'uchoyo' iliyoonyeshwa na baadhi ya wachezaji na kuwa inachangia kuwakosesha ushindi mnono
Nabi ametahadharisha kuwa hatakuwa tayari kumuweka kwenye kikosi chake mchezaji ambaye hashirikiani na wenzake uwanjani
"Ipo changamoto nimeiona katika mchezo wa JKU na nilikuwa mkali katika vyumba baada ya mchezo kumalizika, siku zote inashinda timu anafunga au anatengeneza nafasi mchezaji"
"Tunajua kwamba bado kuna mambo ambayo yanaendelea kujijenga taratibu lakini yapo mazingira ambayo tunapunguza uwezekano wa kutanua ushindi wetu,tunahitaji kuwa na mchezaji anayetambua mahitaji ya timu katika ushindi na sio kuangalia mafanikio yake binafsi," Nabi aliliambia gazeti la Mwanaspoti
Nabi ametumia kipindi cha mapumziko ya Kimataifa kuimarisha kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumanne ijayo mkoani Ruvuma
Baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika michezo minne mfululizo, Wananchi wanataka kuona timu yao ikiongeza idadi ya mabao katika mechi ili kuwa na uhakika wa kuondoka na alama tatu katika kila mchezo