Kesho Jumapili,Β kikosi cha Yanga kitaelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utaigwa Jumanne uwanja wa Majimaji
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria, Nesreddine Nabi amesema anatengeneza kikosi imara kitakachowapa raha mashabiki na wanachama wa timu hiyo
Nabi ameeleza kufurahishwa na kurejea kwa walinzi wa pembeni, David Bryson na Yassin Mustafa ambao walikuwa majeruhi na sasa wameongeza nguvu katika safu yake ya ulinzi.
Alisema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo na hana presha yoyote katika safu ya ulinzi kwa sababu kurejea kwa nyota hao kumeimarisha timu hiyo huku akiwa mkali kwa washambuliaji wake kucheza kwa ushirikiano wenyewe kwa wenyewe.
"Sina presha kwenye safu yangu ya ulinzi tumeimarika vizuri, nimekuwa mkali kwa washambuliaji na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano bila kuangalia mafanikio ya mtu binafsi katika kutengeneza nafasi na kufunga,"alisema Nabi
Yanga imepania kuendeleza kasi ya ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo unaoongozwa na Polisi Tanzania.
"Tumejipanga vizuri na kikosi kipo tayari kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri katika mchezo wetu huo, KMC FC sio timu mbaya, wamejipanga vizuri na nina imani utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa kwa pande zote mbili"
Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na alama sita baada ya kushinda michezo yote miwili. Wako nyuma ya Polisi Tanzania kwa tofauti ya mabao