Chirwa lawamani Yanga kutolewa kombe la Mapinduzi

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
11 Jan 2018
Chirwa lawamani Yanga kutolewa kombe la Mapinduzi
Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amejikuta lawamani baada ya kukosa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya URA jana ambapo yeye pekee ndiye alikosa penati kati ya 10 zilizopigwa.

Penati yake iliyodakwa na mlindalango ilipelekea Yanga ikatolewa kwa panati 5-4 na URA.

Mashabiki wengi wamekuwa wakimlaumu si kwa sababu ya kukosa penati, bali ni kuhoji juu ya uzalendo wake kwa klabu ya Yanga.

Aidha wengi wameshangazwa na benchi la ufundi kumpanga Chirwa kwenye mchezo huo licha ya kwamba hakuwa kambini kwa zaidi ya wiki sita.

Chirwa hahukumiwi kwa kukosa penati. Jambo lolote linaweza kutokea linapokuja swala la changamoto ya mikwaju ya penati.

Na ukweli ni kwamba makocha huwa hawapangi nani apige penati, bali huwauliza wachezaji nani yuko tayari kupiga penati.

Ila kukosekana kwake kikosini kwa muda mrefu huku zikiibuliwa tetesi kwamba aligoma kurejea kushinikiza alipwe pesa za usajili (sio mshahara) alizokuwa anadai hapo ndipo penye tatizo.

Sasa baada ya yote hayo, bado siku unarejea unapangwa katika mchezo muhimu, unacheza chini ya kiwango, unabeba jukumu la kupiga penati, unakosa.

Huwezi kekwepa lawama kwenye mazingira kama hayo.

Bila shaka Chirwa amejifunza jambo kupitia kadhia hii kadhalika naamini benchi la ufundi haliwezi kufanya bahati nasibu kama hiyo tena.

Kuelekea mchezo dhidi ya URA, katika moja ya mahojiano yake, Kocha Msaidizi wa Yanga,Shedrack Nsajigwa alibainisha kuwa Yanga haikuwa na mpango wa kuongeza mchezaji yeyote miongoni mwa wale waliobaki Dar kwa kuwa wana kikosi kipana.

Kwa maoni yangu, hakukuwa na ubaya kwa Chirwa kuongeza kikosini, lakini haikuwa sawa yeye kucheza katika chezo dhidi ya URA.

Kama ilikuwa ni lazima atumike kwenye michuano hiyo basi ingekuwa vyema katika mchezo fainali kama Yanga ingefanikiwa kufuzu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
54m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’