Yanga imetakata uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma leo baada ya kuichapa KMC mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC
Wananchi waliuanza mchezo huo kwa kasi na walianza kuhesabu bao la kwanza kwenye dakika ya 5 likiwekwa kambani na Fiston Mayele akimalizia shuti la Feisal Salum
Yanga iliendelea kulisakama lango la KMC na kwenye dakika ya 12 Feisal Salum akafunga bao la pili kwa shuti kali kutoka nje ya 18
Yacouba Songne angeweza kufunga nafasi nyingine shuti lake likigonga mwamba
Kipindi cha pili Yanga ilicheza kwa tahadhari zaidi lakini ilitengeneza nafasi nyingine kadhaa ambazo hata hivyo hazikuweza kuzaa bao
Yanga imeendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 sasa ikipanda kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 9





ADVERTISE HERE