Jesus Moloko, hii ni winga ya kisasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Oct 2021
Jesus Moloko, hii ni winga ya kisasa

Mashabiki wa Yanga waliumia sana baada ya uongozi kumuuza winga mwenye kasi ya 'umeme' Tuisila Kisinda aliyesajiliwa na RS Berkane ya Morocco

Kisinda alijizoelea mashabiki wengi kutokana na aina yake ya uchezaji, akitumia mbio kama silaha muhimu ya kuwatesa walinzi wa timu pinzani

Huyu mwamba alikuwa anakimbia kwelikweli, kuna mabeki walifanya sherehe baada ya kusikia Yanga wamemuuza!

Lakini Wananchi wamemleta mbadala wake ambaye ni moto zaidi, Jesus Moloko

Moloko ana kasi kama ilivyokuwa kwa Kisinda lakini yeye ni mchezaji anayekimbia kwendana na matukio

Ukimuona anakimbia basi anao mpira mguuni kwake au pasi imewekwa njiani. Mfumo wa timu unaamua mbio zake azitumie vipi!

Ni mchezaji anayejua kuharakisha mashambulizi na anawatengenezea wenzake nafasi

Upande wa kulia anaocheza na Shabani Djuma unaonekana kuwa na madhara zaidi na Kocha Nasreddine Nabi anautumia zaidi kujenga mashambulizi

Moloko anaufanisi zaidi kulinganisha na Kisinda ambaye mipira yake ya mwisho mara nyingi ilikuwa haitabiriki

Ni aina ya mawinga ambao mabeki hawawapendi kwani yeye mashambulizi yake anayaanzia chini kabisa na kukimbia kwa kasi mpaka eneo la hatari

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’