Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' hawaangushi mashabiki wa Yanga ambao wameweka imani kubwa kwake
Katika mechi tatu za ligi, Feisal amehusika katika mabao matatu, amefunga mawili na kutoa 'assist' moja
Kama atabakia katika ubora alionao kwa msimu mzima, huu unaweza kuwa msimu wa maajabu kwake
Kwani amedhihirisha ni mchezaji hatari sana anapokuwa mbele ya uso wa lango la timu pinzani
Kocha Nasreddine Nabi anastahili pongezi kwa kumtumia Feisal katika eneo hilo linalomfaa zaidi, sasa mchango wake unaonekana
Makocha wote waliomtangulia kuanzia Mwinyi Zahera, Luc Eymael, Zlatko Krympotic, Juma Mwambusi na hata Cedric Kaze hawakuwahi kumtumia Feisal katika eneo hilo
Tangu Nabi aanze kumtumia kama namba 10, Feisal amekuwa na wastani wa kufunga au kutengeneza nafasi katika kila mchezo