Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza jana alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Avic Town, Kigamboni
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Saido alionyesha kiwango bora akionekana kumvutia kocha Nasreddine Nabi ambaye alimtumia kama mchezaji kiongozi
Hata bao alilofunga Yusufu Athumani lilitokana na pasi ya nyota huyo wa Kimataifa wa Burundi
Pengine Wananchi wanaweza kumshuhudia katika mchezo ujao dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa


ADVERTISE HERE