Mlinzi wa kushoto wa Yanga Yassin Mustafa juzi alicheza dakika 45 mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania ambao Yanga ilishinda kwa bao 1-0
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Yassin kushiriki tangu alipopata majeraha miezi sita iliyopita
Daktari wa Yanga Dk Shecky Mngazija amesema Yassin yuko timamu kwa asilimia 100 baada ya kukamilisha program za mazoezi alizokuwa akiendelea nazo
"Kwa muda mrefu amekuwa akiendelea na program ya kujiimarisha 'recovery' ambazo amemaliza kwa sasa anaweza kucheza mechi yoyote," alisema Dk Mngazija
Kurejea kwake kumemuongezea machaguo kocha Nasreddine Nabi katika safu yake ya ulinzi upande wa kushoto akiwa Yassin, David Bryson na Adeyum Saleh
Pamoja nao, Kibwana Shomari ambaye alianza kutumika katika eneo hilo wakati wachezaji hao walipokuwa majeruhi, ameendelea kuaminiwa na Nabi