Yanga inaweza kujitengenezea mazingira mazuri katika mbio za ubingwa mapema tu kama itaweza kuibuka na ushindi katika michezo mitano ijayo
Katika mechi hizo Yanga itakutana na wapinzani wake Azam Fc na Simba ambao wanatajwa kuwa katika 'marathon' moja na Yanga
Ni kuanzia Jumamosi hii kwa mchezo dhidi ya Azam FC utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa Saa 1.00 usiku. Kama Yanga itaibuka na ushindi, itaipiku Azam kwa pointi nane kwani hadi sasa wako mbele yao pointi tano
Mchezo utakaofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja huo huo wa Mkapa, Novemba 02, ambapo baada ya mchezo huo, ligi itasimama kupisha kalenda ya michuano ya FIFA kusaka tiketi ya kombe la Dunia
Oktoba 20 Wananchi wataelekea Lindi kuvaana na Namungo FC. Namungo imekuwa ikipunguza alama za Yanga ambapo katika msimu uliopita Yanga iliambulia alama mbili tu kwa michezo yote miwili kuwa sare
Yanga ikimalizana na Namungo FC, mchezo utakaofuata itaenda Mbeya kukabiliana na Mbeya Kwanza, Novemba 30 kwenye Uwanja wa Sokoine na baadae kurejea jijini Dar es salaam kuvaana na watani wao wa jadi, Simba, Desemba 11
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anapaswa kuchanga karata zake vyema kuhakikisha anaondoka na alama zote dhidi ya wapinzani wake katika mbio za ubingwa