Wengi wamekuwa na shauku ya kufahamu nini kimeamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa michezo (CAS) juu ya kesi ya Yanga dhidi ya mchezaji Bernard Morrison ambapo baada ya hukumu kuahirishwa Septemba 21, ilitajwa kuwa itatolewa Oktoba 26
Hukumu ya kesi hiyo ilipigwa kalenda mara mbili, kwa kulingana na taarifa za CAS, mwanzo ilikuwa August 24, ikapelekwa Septemba 21 na ikarushwa Oktoba 26
Jambo moja la uhakika ni kuwa uongozi wa Yanga utatoa taarifa pale watakapopokea hukumu hiyo, ukimya huu unamaanisha bado hawajapokea taarifa ya CAS
CAS ni Mahakama ya Kimataifa, wana utaratibu wao, na wanatoa maamuzi yao pasipo kushinikizwa
Maamuzi ya kesi yanaweza kuchelewa, hili hutokea mara nyingi lakini lazima yatatolewa
Wale wanaouliza maswali humu kuhusu hukumu hiyo inapaswa wasubiri, taarifa LAZIMA itatolewa
Kwa wale wanaoamini Yanga imeshindwa kesi hiyo wajiulize mbona Simba hawajatoa taarifa kuhusu mchezaji wao kushinda?
Ndio maana tunasema hukumu hiyo itafahamika, Yanga ikishinda/ikishindwa itatoa taarifa lakini kama Morrison akishinda LAZIMA Simba watatoa taarifa
Hivyo ni wazi jambo hili bado halijawafikia mezani pande zote, Yanga na Morrison