Ni Yacouba au Saido leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2021
Ni Yacouba au Saido leo?

Leo benchi la ufundi la Yanga litakuwa na mtihani mwingine wa kuamua wachezaji nane wa kigeni ambao wanapaswa kujumuishwa kwenye kikosi kitakachoikbaili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa kuanzia saa moja usiku

Ni mtihani hasa unapokuwa na wachezaji 10 ambao wote wana sifa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza lakini unalazimika kuwaacha wawili nje ili kukidhi matakwa ya kanuni

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema ni jambo gumu lakini ndivyo kanuni inavyowaelekeza, wanalazimika kuifuata

Wachezaji ambao mpaka sasa wamejihakikishia nafasi ya kuingia katika wachezaji nane ni mlinda lango Djigui Diarra, Yannick Bangala, Khalid Aucho na Djuma Shabani

Wengine ni Fiston Mayele, Heritier Makambo na Jesus Moloko

Kati ya Yacouba Songne, Mukoko Tonombe na Saido Ntibazonkiza, wawili kati yao hawatajumuishwa kwenye kikosi leo

Pamoja na kulalamikiwa kuwa anapoteza nafasi nyingi za wazi, Yacouba amekuwa akianzishwa kwenye kikosi cha kwanza kutokana na aina ya uchezaji wake

Ni mchezaji msumbufu ambaye hupendelea kusukuma mashambulizi mbele kila anapopata mpira

Bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kuaminiwa leo licha ya wengi kutamani kuona Saido akipewa nafasi yake

Saido alionyesha kiwango bora kwenye mchezo wa kirafiki ambao Yanga ilicheza karibuni dhidi ya JKT Tanzania, akitoa pasi ya bao lililofungwa na Yusufu Athumani

Bado itakuwa ngumu kwa Mukoko kuwatenganisha Bangala na Aucho ambao wametengeneza pacha bora sana kwenye eneo la kiungo

Kwa sasa Nabi hana sababu ya kutumia Bangala kwenye safu ya ulinzi kwa kuwa nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto yupo

Aidha Bangala akicheza kiungo anaifanya Yanga kuwa imara zaidi katika eneo hilo pengine kuliko hata akicheza kwenye safu ya ulinzi

Hii Yanga ya sasa ukipewa upange kikosi unaweza kuchanganyikiwa...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’