Kikosi cha Yanga kesho Jumanne kitashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ruvu Shooting katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC mzunguuko wa tano
Baada ya kuifunza soka Azam Fc, Wananchi wanaelekeza silaha zao kwa Ruvu Shooting, hii ni fainali nyingine
Vijana wa Kocha Nasreddine Nabi wanasaka ushindi wa tano mfululizo ili kuendelea kujichimbia kileleni kwenye msimamo wa ligi
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki kufurika kwa wingi pale kwa Mkapa kushuhudia 'pira burudani' kutoka kwa timu yao
Aidha Bumbuli pia amewaalika watani zake Simba wafike waondoe 'stress' kutokana na maumivu wanayosababishiwa na timu yao
Jana Simba ilishindwa kutamba mbele ya Coastal Union baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Coastal Union ni moja ya timu zilizokuwa zikiwapa Simba mtaji wa mabao katika misimu iliyopita, lakini jana waligoma