Kutakuwa na mapumziko ya wiki mbili baada ya mechi za raundi ya tano kupisha kalenda ya michuano ya FIFA kusaka nafasi ya kucheza kombe la Dunia kule Qatar
Kikosi cha Yanga kitarejea tena dimbani Novemba 20 kwa mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa mkoani Lindi katika uwanja wa Ilulu
Utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga kucheza nje ya jiji la Dar es salaam wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kule Kaitaba na pia kushinda mabao 2-0 dhidi ya KMC kule Ruvuma
Kocha Nasreddine Nabi atakuwa na wiki nyingine mbili kukiimarisha kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Namungo
Yanga bado haijaweza kupata ushindi dhidi ya Namungo Fc katika misimu miwili ambayo timu hizo zimekutana kwenye ligi
Hata hivyo msimu huu Wananchi wamepania kuvunja 'miiko' yote