Baada ya mapumziko ya siku mbili kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea dimba la Uhuru keshokutwa Jumapili kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mwadui FC.
Mchezo huo wa mzunguuko wa 13 utapigwa Jumatano, Januari 17, 2018 kwenye uwanja huo.
Baada ya kutolewa na URA katika hatua ya nusu fainali kombe la Mapinduzi, kikosi cha Yanga kilichowasili jijini Dar es salaam jana kilipewa mapumziko ya siku mbili.
Yanga inahitaji kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Mwadui FC ili kupunguza tofauti ya pointi baina yake na timu za Simba, Azam FC na Singida United zinazokabiliwa na michezo migumu.
Simba itachuana na SIngida United Alhamisi, Januari 18 wakati siku hiyohiyo Azam FC itakuwa ugenini mkoani Ruvuma kuivaa Majimaji

ADVERTISE HERE