Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa klabu ya RS Berkane bado inamuhitaji kiungo Mukoko Tonombe ambaye walijaribu kumsajili katika dirisha lililopita
Katika usajili uliopita Berkane inayonolewa na Florente Ibenge aliyewahi kuwa kocha wa AS Vita, iliwasilisha ofa kwa klabu ya Yanga kuwataka Tuisila Kisinda na Mukoko
Yanga ikaridhia kumuuza Kisinda lakini wakaweka ngumu kwa upande wa Mukoko
Lakini wakati huu Yanga inaweza kusikiliza ofa ya Berkane na pengine kumruhusu Mukoko kujiunga na timu hiyo lakini kuna sharti ambalo Berkane watapaswa kuliafiki!
Kuna mchezaji kutoka RS Berkane Yanga inamuhitaji, na wadhamini GSM wako tayari kumtumia Mukoko katika dili hiyo
Zipo taarifa kuwa kuna makubaliano yamefikiwa na mchakato wa usajili huo utakamilishwa kwenye dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa Disemba 15 (Mwezi ujao)
Msimu huu Yanga imedhamiria kushinda ubingwa wa ligi kuu na zaidi kuwa na kikosi imara ambacho kitafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao