Nabi amepania kuendeleza moto wa ushindi ligi ikirejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2021
Nabi amepania kuendeleza moto wa ushindi ligi ikirejea

Yanga imerejea mazoezini kuanda maandalizi ya mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa mkoani Lindi Novemba 20

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema ataendelea kuwaimarisha wachezaji wake kwa sababu wanahitaji kupata pointi tatu katika kila mechi watakayocheza kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara

Nabi amesema mpaka sasa timu yake imefanya vizuri kwa kushinda michezo yote mitano lakini amekiri haikuwa kazi rahisi kwa nyota wake kuvuna pointi 15 ambazo zimewaweka katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16

"Nina furaha, unapocheza mechi tano na zote ukapata ushindi, wote tunajua ligi ni ngumu, ina ushindani, timu zote zimejipanga kusaka pointi, kwa sababu hiyo hatutazubaa, tunahitaji kuona tunazidi kuimarika,” alisema Nabi

Kocha huyo aliongeza ligi bado iko katika hatua za mwanzo, hivyo wanahitaji kuendelea kufanya vizuri kwa ajili ya kutimiza malengo yao kama ambavyo timu nyingine zilivyojipanga.

"Kila timu imejipanga, tumeanza msimu vizuri, tunahitaji kuendelea hivi hivi, tunakutana na changamoto ya kucheza kwenye viwanja tofauti, lakini hili tunakutana nalo wote, huwezi kulizungumzia, kikubwa ni kuendelea kupambana ili kupata kile tunachokitarajia," Nabi alisema

Aliongeza ushindani wa namba kwenye kikosi chake unasaidia kuimarisha ubora wa timu na licha ya kupata ushindi kwenye mechi walizocheza, bado hakuna mchezaji mwenye uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.

"Kila mchezaji ana ubora wake, kupata nafasi ya kucheza au kutopata ni suala la wakati, kikosi kitakachoanza kinatokana na mfumo na aina ya mpinzani tunayekutana naye, kuna mchezaji mwingine anakuwa bora anapokutana na timu A, lakini huyo huyo anakaa nje unapocheza na timu B"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’