Senzo awakemea wanaoshambulia GSM

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Nov 2021
Senzo awakemea wanaoshambulia GSM

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amewakemea wanahabari walioanzisha mijadala yenye lengo la kuwakatisha tamaa wawekezaji wanaojitoa kukuza soka la Tanzania, GSM ikiwa imelengwa zaidi

Aidha Senzo amezitaka Mamlaka za usimamizi wa soka nchini kutokalia kimya mijadala hiyo iliyoanzishwa kwa malengo maovu

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Senzo ametoa maoni yake kuhusu mijadala hiyo;

"Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunasoma mijadala inayomshambulia Mfadhili wetu na mdhamini wetu bila sababu za msingi"

"Mtazamo ambao unaonyeshwa na wafanyakazi wengi wa vyombo vya habari na watu binafsi kuelekea watu wenye sifa nzuri wanaoleta pesa kwenye soka lazima ulaaniwe"

"Haiwezekani kuwa katika nyakati hizi za majaribu ambapo wafadhili hawajitoi sana kudhamini soka na tuna watu binafsi wanaoshambulia watu wale wale ambao wanatumia pesa zao kusaidia soka"

"Je, ni kwa sababu Yanga imeimarika na kufanya vizuri chini ya ufadhili wa GSM ndiyo maana watu wanaona kuna haja ya kumshambulia mfadhili wetu?"

"Natahadharisha ujinga huu na kushauri kwamba ushughulikiwe mara moja na vyombo vinavyohusika na michezo. Kuna ubaya gani kwa GSM kusaidia vilabu vingine vinavyohitaji usaidizi?"

"Hoja wanazotoa ni dhaifu sana zenye lengo la kuleta usumbufu na hofu kwa GSM. Mdhamini wetu endelea na kazi hiyo nzuri na tuendelee kuunga mkono GSM. Kama Yanga, tunashukuru kwa msaada wako wa kifedha kwa klabu"

"Kinachoendelea ni dalili kuwa brand ya GSM inakua na inawasumbua wengine huko sokoni naomba watu waiunge mkono GSM kwa uwekezaji kwenye soka ambayo ni moja ya nguzo muhimu za kijamii katika ustawi wa Tanzania"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’