Nabi 'ampa tano' kocha wa viungo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2021
Nabi 'ampa tano' kocha wa viungo

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema matunda ya kazi nzuri inayofanywa na Kocha wa viungo Helmy Gueldish yameanza kuonekana

Gueldish alitua Yanga akitokea klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia ikiwa ni pendekezo la Nabi mwenyewe

Katika michezo mitatu ya mwanzo wa msimu, kulikuwa na ukosoaji kwa kikosi cha Yanga kuwa 'kinakata upepo' katika kipindi cha pili

Hata hivyo kelele hizo hazisikiki tena baada ya kazi ya Gueldish ambaye amewajenga vyema wachezaji kutokana na mazoezi anayowapatia

Nabi amesema alifahamu ujio wa Gueldish utakuwa na manufaa kwa timu ndio maana alipendekeza kocha huyo apatikane kwa gharama yoyote

"Nilikuwa namwambia kila kitu kwamba mashabiki wanalalamika kwamba eti timu inapungua pumzi akawa anakasirika alijua kwamba muda ambao aliniambia wachezaji watakuwa tayari ulikuwa haujafika na wala Yanga haikuwa inakata pumzi," Nabi alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Huyu ni kocha bora ambaye anajua kutengeneza ufiti wa wachezaji na anaijua kazi yake kuliko watu walivyodhani na sasa kazi yetu kama makocha inakuwa fupi kuingiza mbinu kitu ambacho sasa kinakamilisha kazi yetu hapa"

Mbali na ubora wa Gueldish katika mazoezi ya viungo,  pia anajua kuchambua ubora wa wapinzani kazi ambayo anaifanya kuelekea kila mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’