Kikosi cha Timu ya Wananchi kimeondoka jijini Dar es salaam kwenda Zanzibar kwa ajili mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo unafuata wa Ligi Kuu NBC
Leo usiku Yanga itacheza na Mlandege kwenye Uwanja wa Aman kuanzia saa 2.15 usiku
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wameelekea visiwani Zanzibar na kikosi cha wachezaji, 17 wakiwa wachezaji wa kikosi cha kwanza na wengine watano kutoka timu ya vijana
Yanga inawakosa wachezaji 10 ambao wameondoka kwa ajili ya majukumu ya timu za Taifa huku mshambuliaji Yacouba Songne akiwa ni majeruhi
ADVERTISE HERE