Michuano ya kombe la Mapinduzi kufika tamati leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
13 Jan 2018
Michuano ya kombe la Mapinduzi kufika tamati leo
Saa mbili na robo usiku mabingwa watetezi wa michuano ya michuano ya kombe la Mapinduzi, Azam FC watashuka kwenye dimba la Amani kujaribu kutwaa taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo watakapowavaa watoza ushuru wa Uganda, URA.

Michuano hiyo iliyoanza Disembe 29, 2017 inafika tamati leo kwa mchezo huo wa fainali.

Azam FC na URA zinakutana kwa mara ya pili kwenye michuano hiyo kwani zilikuwa kundi moja, A.

Katika hatua ya makundi URA iliichapa Azam FC bao 1-0 na hivyo kuufanya mchezo huo uwe wa kisasi kwa Azam FC.

Wakati michuano hiyo ikifikia tamati leo, wadau wa soka wameshauri michuano ijayo ifanyiwe marakebisho katika upangaji wa ratiba

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ameshauri uapatikane utaratibu mzuri wa kuendesha michuano hiyo bila kuathiri afya za wachezaji.

Mkwasa amesema kucheza mechi mfululizo katika michuano hiyo si jambo zuri kwa wachezaji kiafya.

“Wanaweza kuweka utaratibu mzuri katika michuano ijayo ili kuwaepusha wachezaji kucheza mechi nyingi sana mfululizo katika kipindi kifupi,” alisema Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha.

“Wakae waliangalie hili kwa faida ya wachezaji ambao pia wanakuwa wana majukumu baada ya michuano hii.”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →