Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne raia wa Burkina Faso, anaweza kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya goti aliyopata
Yacouba aliumia kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Yanga ilishinda mabao 3-1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yacouba ameshindwa kujiunga na timu ya taifa ya Burkina Faso kutokana na majeraha hayo ambapo tayari ameanza matibabu
Mmoja wa wachezaji waliokuwa wamejihakikishia namba kwenye kikosi cha Kocha Nasreddine Nabi ambaye sasa analazimika kupata mbadala wake
Yanga ina wachezaji wengi katika nafasi yake kama mkongwe Saido Ntibazonkiza, Farid Mussa, Deus Kaseke, Yusuf Athuman, Ditram Nchimbi na Dickson Ambundo ambaye kwa sasa yuko nje ya uwanja akiuguza jeraha la mkono
ADVERTISE HERE