Kikosi cha Yanga leo kinakamilisha mechi ya kirafiki visiwani Zanzibar kwa kuikabili KMKM katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Amaan, saa mbili na robo usiku
Yanga ilialikwa Zanzibar kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja wa Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ambapo Jumanne ilicheza mechi ya kwanza dhidi ya Mlandege Fc na kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Wananchi waliweka kambi visiwani Zanzibar leo wakihitimisha mchezo wao wa pili
Yanga pia inatumia michezo hiyo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Novemba 20 katika uwanja wa Ilulu, Lindi
ADVERTISE HERE